AMBER LULU ABANWA, SKENDO YA UKUWADI WA MAMODO…!!

VIDEO Queen aliye ‘hot’ Bongo, Lulu Auggen ‘Amber Lulu’ anadaiwa kuwakuwadia mastaa wenzake kwa mapedeshee kiasi cha kuwa maarufu kwa jina la wakala wa Ma-video Queen ‘mamodo’.

amber_lulu amber_lulu2 amber_lulu3

Mmoja wa warembo aliyeomba jina lake lihifadhiwe alisema kuwa, mwanadada huyo amekuwa akifanya mchezo huo kwa muda mrefu kiasi cha kujiingizia kipato kikubwa.

“Yule namjua vizuri, aliwahi kuniunganisha na jamaa mmoja ambaye nilimkubalia kutokana na njaa zangu, hee! Siku nyingine si akanipigia tena kuniambia eti kuna mtu ananihitaji, nikajua ni kuwadi,” alisema mtoa habari huyo.

Katika kupata ukweli wa madai hayo, paparazi wetu alimtafuta Amber Lulu, alipopatikana na kubanwa alisema: “Ni kweli wapo watu wananipaga dili za kuwaunganisha na mastaa, sasa nitaachaje hela wakati maisha yenyewe ndiyo haya.”

“KWA NINAYOYAONA, SITAMANI NDOA” – MARY MAWIGI…!!

MSANII wa filamu za Kibongo, Mary Mawigi amesema kuwa tofauti na wanawake wengine wanaotamani ndoa, yeye hafi kirii kabisa suala hilo kutokana na jinsi anavyoona baadhi ya wanawake wanavyolia na kujuta kuolewa.

mary_mawigi mary_mawigi2

Akipiga stori na paparazi, Mary alisema kuwa huenda watu wakamshangaa kwa kusema hivyo lakini ndiyo ukweli kwani idadi kubwa ya wanawake hawana furaha ya ndoa kutokana na sarakasi zilizomo ndani yake, hivyo yeye atabaki kuwa singo.

“Wapo marafiki zangu ambao walililia sana ndoa, hatimaye wakaolewa lakini sasa hivi wanatamani kutoka kutokana na kile wanachokiona, mateso na manyanyaso vinatawala, mimi ndoa noo kwa kweli,” alisema Mary.

MADAI…‘MATITI YA KAJALA, DAWA ZA KICHINA ZAHUSIKA’…!!

Baada ya gumzo kubwa kuibuka juu ya muonekano mpya wa matiti ya msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja, shostito wake wa karibu amemwaga ubuyu kuwa, dawa za kuongeza matiti za Kichina zinahusika.

kajala

Akipigia stori na paparazi hivi karibuni, mtoa ubuyu wetu ambaye aliomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, huko nyuma matiti ya Kajala yalikuwa ‘ndala’ akawa anatumia dawa f’lani za kupaka ili kuyafanya yatune.

“Nyie muoneni vile tu lakini zile nido zake za sasa Mchina anahusika sana, hawezi kuanika ukweli lakini habari ndiyo hiyo,” alisema mtoa ubuyu huyo.

Paparazi wetu alibahatika kuongea na Kajala juu ya madai hayo ambapo alisema: “Watu bwana wanaongea sana, je nikiamua sasa kutumia hizo dawa itakuwaje? Niseme tu kwamba matiti yangu ni orijino na siku zote yana mvuto ndiyo maana sionagi hatari kuyaanika.

WEMA AFUNGUKA BAADA YA KUCHOSHWA NA MAJUNGU YA WATU…!!

Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ameonesha kuchoka na maneno mbalimbali kutoka kwa watu hususani kwenye mitandao ya kijamii kiasi cha kuamua kutoa yake ya moyoni kwa watu wote ambao wamekuwa wakimfuatilia maisha yake.

wema_sepetu1 wema_sepetu2

Ameonesha kukasirishwa na baadhi ya watu wanaomsema kwenye mitandao ya kijamii hususani kuhusu mapungufu yake.

Wema Sepetu ametumia mtandao wake wa Instagram kuweka ujumbe mrefu kwa watu hao, huku akiwataka wamuache aishi maisha yake kwani hajawahi hata siku moja kwenda kuomba msaada kwao, na kusema hata siku atakapokufa atakufa mwenyewe na kama ni majibu kwa Mungu atajibu mwenyewe.

“Naomba niseme kitu na nieleweke tafadhalli, sijawahi hata siku moja kwenda kwa hata mmoja wenu na kumgongea kuomba hata hela ya chumvi. Maisha yangu yananihusu mimi na hata siku nikifa nakufa mwenyewe, majibu kwa Mungu naenda kujibu peke yangu. Niacheni jamani nimechoka” aliandika Wema Sepetu

Mbali na hilo Wema Sepetu amewataka watu ambao wanakereka na aina ya maisha ambayo yeye anaishi waache kuyafuatilia kwani si lazima kufuatilia kile akifanyacho au maisha anayoishi yeye.

“Kama nakukera na maisha yangu basi usiyafuatilie siyo lazima. Nisiheme sasa jamanii. Naomba tafadhari kama mapungufu ni ya kwangu mimi. Niacheni mimi nafanya kile kinachoridhisha nafsi yangu maana sipendi kujikasirisha. Kwani nikitajirika mimi au nikiwa masikini wewe unapata faida gani. Jiulize kwanza hilo swali ndiyo uanze kutoa maneno yako” alisema Wema Sepetu

“KWA SASA SITAKI TENA KUJIINGIZA KATIKA BONGO MOVIE” – SINTAH…!!

Mkali wa zamani wa maigizo, Sintah ambae alitamba na skendo kibao kipindi hicho na unaambiwa yeye ndiyo wa kwanza kuwa na skendo kubwa Bongo, amefunguka na kueleza kwa sasa ana ishu gani mjini.

sintah sintah2

Sintah ambaye alikuwa pia muigizaji mahiri anasema “Kwa sasa sitaki tena kujiingiza katika bongo movie najishughulisha na biashara zangu binafsi na nipo katika hatua za mwisho kukamilisha lebo yangu ya wasanii wa bongo fleva.”

Hata hivyo Sintah alimalizia kwa kusema kwa sasa anawaachia machipukizi wanaoibukia katika bongo move nao kufanya vizuri na kusongeza saana ya bongo na pia hataki tena maswala ya skendo za aina yeyote huku akisema kwa sasa anamsimamia msaniianayejulikana kwa jina la Tino ndo ambaye taari yupo katika lebo yake.

Chanzo: eatv

PICHA: BATA ZA JUX NA VANESSA MDEE KATIKA MBUGA YA SERENGETI…!!

Wanamuziki, Vanessa Mdee na mpenzi wake Juma Jux ‘Jux’ baada ya manenomaneno kuzagaa kuwa wameachana juzikati wapenzi hao walionekana kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti iliyopo mkoani Mara kisha kwenda kula bata kwenye hoteli ya bei mbaya ya Singita.

vanessa_mdee vanessa_mdee2

Akipiga stori na paparazi juzi akiwa Serengeti, Vanessa alisema kuwa, wameamua kwenda huko kwa mapumziko ya siku nne ikiwa ni sehemu ya kufanya utalii wa ndani na wamekula bata za kutosha.

“Ni mambo ya utalii wa ndani, tumekuja huku kupumzika kidogo, siyo lazima kwenda nchi za nje kwa mapumziko, humuhumu Bongo kuna sehemu unakwenda na unajisikia furaha,” alisema mwanadada huyo.

vanessa_mdee3 vanessa_mdee4

Singita ni hoteli ya kifahari iliyopo mkoani Mara ambayo inaiingizia nchi fedha nyingi za kigeni.

Wanamuziki, Vanessa Mdee na mpenzi wake Juma Jux ‘Jux’ baada ya manenomaneno kuzagaa kuwa wameachana juzikati wapenzi hao walionekana kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti iliyopo mkoani Mara kisha kwenda kula bata kwenye hoteli ya bei mbaya ya Singita.

Akipiga stori na safu hii juzi akiwa Serengeti, Vanessa alisema kuwa, wameamua kwenda huko kwa mapumziko ya siku nne ikiwa ni sehemu ya kufanya utalii wa ndani na wamekula bata za kutosha.

“Ni mambo ya utalii wa ndani, tumekuja huku kupumzika kidogo, siyo lazima kwenda nchi za nje kwa mapumziko, humuhumu Bongo kuna sehemu unakwenda na unajisikia furaha,” alisema mwanadada huyo.

Singita ni hoteli ya kifahari iliyopo mkoani Mara ambayo inaiingizia nchi fedha nyingi za kigeni.

MREMBO TUNDA AFUNGUKA KUMWAGANA NA RAPPER YOUNG D…!!

MUUZA nyago macha-chari Bongo, Tunda Sebastian amefunguka kumwagana na mwandani wake wa muda mrefu, ambaye ni staa wa Bongo Fleva, David Genzi ‘Young D’ na kusema ameamua kujiweka kando kwenye maswala ya mapenzi.

tunda tunda2

Akipiga stori na paparazi baada ya kumbananisha kuhusiana na tetesi za uhusiano wake kuvunjika kutokana Young D kubaini anatoka na mwanamuziki mwenziye (jina kapuni) ndipo akaeleza kuwa, ishu hiyo haina ukweli ila ameachana na mwandani wake huyo kwa sababu ambazo hawezi kuzianika kwa sasa.

“Hayo ya kutoka na huyo msanii si kweli na kuhusu Young D nimeshaachana, sifikirii kuwa na msanii yeyote na sihitaji mpenzi kwa sasa,” alisema.

AUNT EZEKIEL AKIMBILIA GYM KUNUSURU PENZI…!!

Staa wa filamu, Aunt Ezekiel aliye katika mapenzi na dansa Moses Iyobo, ameamua kukimbilia gym kwa ajili ya kupunguza unene unaomuandama ili kulinusuru penzi lake.

aunt_ezekiel

Akizungumza na paparazi, Aunt amesema ameanza mazoezi ya nguvu kila asubuhi ili aweze kupunguza mwili aendane na mpenzi wake kwani mwili wake ni mkubwa kuliko wa mwenzie.

“Daah, nimeona nitapoteza penzi langu bure, nimekuwa mnene kumpita baby kitu ambacho siyo sawa, nilikuwa na kilo 87, hivi sasa nimepunguza kilo sita,” alisema.

ALIYEMTOA BARAKA DA PRINCE KIMUZIKI AFUNGUKA YA MOYONI BAADA YA KUCHUKULIWA NA ROCKSTAR 4000…!!

Aliyemtoa Baraka Da Prince kupitia rekodi yake ya JitunzeKidbway ameongelea uhamaji wa Baraka kwenda RockStar 4000 nakusema ni njia nzuri kama atafikia malengo aliyojiwekea.

kidbway

KidBway anasema “Nitafurahi akifikia yale malengo niliyokuwa nayo kichwani wakati naanza kufanya naye kazi, hata kama atayafikia kwenye njia tofauti na nilizoona mimi ,nitafurahia kwa mafanikio yake kama ndio njia itakayomfikisha”

Pia Kid amesema “Muda mwingine unatakiwa kujitoa hata kama utaumiza watu ili ufanikiwe, siwezi mtakia mabaya,sio vizuri kumuombea mtu vitu vibaya”.

JAY MOE AFUNGUKA KUTOKA KIMAPENZI NA SHILOLE…!!

Mwanamuziki rapa nchini anayetikisa kwa ngoma ya ‘Pesa Madafu’, Jay Moe amekuwa akionekana karibu sana na rapa Bilnass ambaye anatikisa na ngoma ya ‘Chafu Pozi’ kitu ambacho ni njia pekee ya Jay Moe kumpata mrembo Shilole.

shilole

Baada ya kuwepo kwa tetesi za wawili hao kutoka kimapenzi na zaidi kuonekana picha wako pamoja kwenye moja ya eneo za kula bata wakati wa usiku, ENewz ilimtafuta rapa Jay Moe avunje mzizi huo wa fitna kama ni kweli anaanguka kwa Shilole lakini alikanusha nakusema ndio mara ya kwanza yeye kusikia habari hizo.

“Ndio kwanza nasikia mambo hayo, sijui mamneno hayo yametoka wapi, ni mambo ya muziki tu na uvumi wa stori tofauti, kama picha mimi ni msanii na kama wasanii picha ni kawaida tu ila hakuna kinachoendelea kati yangu na Shilole”

jay_moe

Jay Moe anatajwa kuwa karibu na Shilole kutokana na urafiki wake na Billnas.

MSHINDI WA MISS TABATA 2016 HUYU HAPA…!!

WIKI iliyopita mrembo Grace Malikita alishinda Taji la Miss Tabata mwaka 2016 kwa kuwapiga chini warembo 15 wengine, huku nafasi ya pili akishika Nasra Munna na nafasi ya tatu ikinyakuliwa na Mariam Maabadi.

miss_tabata miss_tabata2 miss_tabata3 miss_tabata4

Shindano hilo lililofanyika Ukumbi wa Dar West Park uliopo Tabata jijini Dar, warembo wengine waliofanikiwa kuingia Tano Bora ni Sabrina Kipuga, Jackline Evarest na Neema Makwaia.

Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Global Publishers likisindikizwa na burudani ya muziki wa dansi kutoka kwa bendi kongwe ya Tanzania African Stars ‘Twanga Pepeta’ pamoja na wasanii wengine.

chanzo: gpl

KAMBI YA LOWASSA YAMFUNGUKIA JACKLINE WOLPER…!!

Kambi ya aliyekuwa Mgombea Urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa tiketi ya Chadema, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa imemfungukia muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper, siku chache tu baada ya kutangaza kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma.

jackline_wolper

Wakizungumza na Risasi Mchanganyiko kwa nyakati tofauti juzi jijini Dar es Salaam, wasemaji wa kambi hiyo walisema alichokifanya Wolper ni utashi wake wa kisiasa, unatokana na hisia zake, ingawa pia walimsema kama mtu asiyefahamu misingi, sera, itikadi, imani wa ilani za Chadema.

Msemaji binafsi wa Lowasa, Aboubakary Liongo, aliliambia gazeti hili kuwa ni vigumu kwa kiongozi huyo kumzungumzia Wolper kwa sababu hakukuwahi kuwa na ‘connection’ ya moja kwa moja baina yao, isipokuwa msanii huyo alijiunga na wanamabadiliko kwa utashi wake mwenyewe.

“Mzee hawezi kumzungumzia, alikuja huku kama ambavyo vijana wengine wengi walikuja wakifuata mabadiliko, kama kuna wa kumzungumzia, labda ni viongozi wa chama kwa sababu operesheni zote zilizokuwa zikifanywa wakati ule, ziliratibiwa na chama.

Wao ndiyo wanaweza kuwa na la kusema kuhusu yeye, ila ninachokiona mimi ni kuwa Wolper ni mtu mzima, mwenye akili timamu, alikuja kwa utashi wake na kama anaondoka, pia anafanya hivyo kwa utashi wake,” alisema Liongo, ambaye ni mtangazaji mwandamizi wa redio nchini.

Kwa upande wake, msemaji wa Chadema, Tumaini Makene, alisema Wolper ni mtu asiye na msimamo, asiyeelewa misingi, ilani, sera wala itikadi za Chadema, ndiyo maana haelewi nini anafanya.

“Sisi tuko na watu wanaoishi kwa matendo, siasa ni maisha ya binadamu, mtu ‘siriaz’ anajua misingi, itikadi, falsafa, imani na ilani za chama chake, hawezi kuwa leo anaamini hivi kesho vile, ukiona mtu kama huyo, ujue hana msimamo, anayumbishwa na ni mtu anayefuata mkumbo,” alisema Makene.

Msemaji huyo alitolea mfano wa vyama viwili vikubwa vya siasa nchini Marekani, Republican na Democrat, akidai waumini wa taasisi hizo mbili za kisiasa, ni watu wenye weledi wanaojua nini wanafuata, hivyo siyo rahisi kuona mtu akihama ovyo kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

jackline_wolper4

Wolper ambaye aliwahi kuwasuta waigizaji wenzake walioamua kujiunga na CCM kwenye kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, akisema ni watu wasioitakia mema taifa kwa kushindwa kuungana ili kulikomboa, hivi karibuni alitangaza kurejea chama tawala, akisema anarudi nyumbani kwani alipotea njia.

“Nimerudi na sifikiri tena kugeuka nyuma, nimeona jinsi rais wetu anavyopigana na chama hiki kuwakomboa wanyonge na sasa hivi kina kasi ya ajabu na nitaendeleza niliyoyaacha,” alisema msanii huyo wakati wa hafla ya kumuaga Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma.

MSANII WA FILAMU GABO ZIGAMBA AFUNGUKA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA FAIZA ALLY…!!

Msanii wa filamu Gabo Zigamba, amefunguka kwa kusema kuwa hana mahusiano yoyote na msanii mwenzake wa kiwanda cha filamu Bongo, Faiza Ally.

msanii_gabo

Muigizaji huyo ambaye hivi karibuni amefanikiwa kushinda tuzo ya mwigizaji bora wa kiume kwenye tamasha la Ziff 2016, ameiambia Times FM kuwa hakuna mahusiano yoyote ya kimapenzi yatakayotokea kati yake na Faiza.

“Faiza namjua kama producer wangu, amenishirikisha kwenye filamu yake ya Baby Mama Drama. Hakuna chochote wala hayatotokea mahusiano ya kimapenzi kati yetu,” amesema Gabo.

DAYNA NYANGE AKANA KUTOKA NA BILLNAS…!!

STAA wa Muziki wa Bongo Fleva, Mwanaisha Said ‘Dayna Nyange’ amemfungukia staa wa Hip Hop Bongo, Billnas kuwa hakuna uhusiano wowote wa kimapenzi unaoendelea kati yao zaidi ya kazi ya kimuziki.

dayna_nyange

Akichonga na paparazi, Dayna anayebamba na Ngoma ya Komela alisema kuwa awali hakuwa akimjua Billnas lakini baada ya kumuona kwa mara ya kwanza kipindi cha nyuma katika Studio za Free Nation kwa Prodyuza T. Touch ndipo walipoanza kujuana.

“Siku moja nilimpigia simu, alikuwa Sauz (Afrika Kusini) kwa shughuli zake za kisanii, nikamwambia nahitaji kufanya ngoma naye. Alikubali na kuanzia hapo tukawa karibu ila kikazi tu, yeye ana uhusiano wake na mimi kivyangu,” alisema Dayna.

MUBENGA AWATEMA OMMY DIMPOZ NA NEDY MUSIC…!!

Aliyekuwa meneja wa Poz kwa Poz (PKP) maarufu kwa jina la Mubenga ameongea na Enews na kusema kuwa sasa hafanyi tena kazi na mwanamuziki Ommy Dimpoz pamoja na Nedy na kwamba sasa anaendelea na kazi zake mwenyewe.

mubenga

Mubenga amesema “Kwa sasa najipanga ili kuja na kampuni yangu ambayo itaitwa Bengaz Entertainment ambayo itakuwa inahusika na maswala yote ya burudani, hivyo wadau wangu waelewe kwamba kwa sasa sifanyi kazi tena na pozi kwa pozi”.

Hata hivyo Mubenga hakuweka wazi sababu iliyopelekea yeye kuachana na PKP huku akisisitiza kuwa anarudi katika kazi zake alizokuwa akizifanya kabla ya kuungana na pozi kwa pozi.

chanzo: eatv

“MIMI NA ESMA HADI KIAMA” – PETIT MAN…!!

Mume wa dada wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Platnumz, Hamad Manungwa ‘Petit Man’ amefunguka kuwa watu wanachonga juu ya uhusiano wake na mzazi mwenzie huyo lakini ndiyo ameshanasa hadi kiama.

esma_platnumz

Akizungumza na mwandishi, Petit Man alisema kuwa ameona bora kukaa na kutulia na mwanamke wake huyo ambaye wamezaa mtoto mmoja wa kike waliyempa jina la Taraj kwa sababu kwingine ni kujitafutia ‘stress’ ambazo hazina sababu za msingi.

esma

“Najua kuna watu wanachonga sana juu ya uhusiano wangu na Esma lakini kiukweli wanune, wanenepe, wavimbe lakini ndiyo nimeshamaliza hapo hadi kiama,” alisema Petit aliyemwagana na Esma kisha kurudiana.

Aliongeza kuwa, hivi sasa wameungana na kuongeza nguvu zaidi ya kufanya kazi za burudani ili kuandaa maisha mazuri ya mtoto wao.

chanzo: gpl