
Yafuatayo ni majina ya washindi wa tuzo za filamu kwa mwaka 2012/13 toka kampuni ya Steps Entertainment zilizofanyika juzi usiku kwenye ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl iliyopo ubungo jijini Dar es Salaam.
Katika tuzo hizi marehemu Steven Kanumba aling’ara kwa kupata tuzo nyingi kuliko waigizaji wote kwa kupata tuzo tatu.
Mwigizaji bora wa kiume ni JB [...]
Muigizaji wa filamu nchini Jaji Khamis ‘Kashi’ amefariki dunia leo mchana katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Kashi amewahi kutamba na mchezo wa ITV, ‘Tamu Chungu’ akiwa na wasanii wenzake kama Mzee Masinde, Samson na wengine.
Mume wa Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki, Khadija Omar Kopa, aitwaye Jaffari Ally amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Marehemu alikuwa anasumbuliwa na matatizo katika mfumo wa upumuaji na mpaka mauti yanamfika alikuwa amelazwa katika hospitali ya wilaya Bagamoyo.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen.
TAKRIBAN wiki moja baada ya kumaliza eda tangu alipofariki mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Januari 2, mwaka huu, staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma anagombewa na midume ikitaka kumuoa.
Akizungumza na mwandishi akiwa nchini Oman, Wastara alifunguka kuwa tangu amalize eda yake hiyo amekuwa akipata usumbufu mkubwa kutoka kwa wanaume mitandaoni na wanaomtamkia mwenyewe.
“Jamani [...]
MWIGIZAJI Mahiri wa filamu Wema Abraham Sepetu ndiye msanii anayelipwa fedha nyingi kuliko msanii yoyote wa filamu katika kushiriki katika filamu kutoka kwa watayarishaji wengine ili uweze kumshirikisha Wema Sepetu katika filamu yako kama mwigizaji bila kujali anacheza scene ngapi gharama yake ni milioni kumi.
Wema ambaye kwa sasa anamiliki kampuni yake ya utengenezaji wa filamu [...]
Baada ya story ya mwanadada Jacqueline wolper kutolewa nje pamoja na vitu vyake kuzagaa kwenye vyombo vya habari hususani magazeti, tuliamua kumtafuta mwanadada huyu ili tupate ukweli wa jambo hilo na kuamua kumtafuta hewani
Mwandishi: Mambo Jack, mzima wewe?
Jackline Wolper: Mi mzima, vipi salama?
Mwandishi: Salama kabisa, vipi kuhusu hii habari ya kutolewa vitu nje ya nyumba? [...]
Katika kuonesha kwamba bado ana kiu ya kuona sanaa yake inapanuka na kuvuma mbali huku akiboresha maisha yake, kukuza kipato na kuongeza ufanisi , msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini H. Baba ameamua kujikita katika biashara kwa style ya kipekee kwa kuingiza sokoni bidhaa aina ya pipi zenye jina, picha na chata [...]