
Marehemu Steven Charles Kanumba (pichani), enzi za uhai wake.
HABARI zisizo rasmi zinasema kwamba kifo cha Kanumba kimetokana ugomvi na mpenzi wake Elizabeth Michael maarufu kama Hot Lulu, kwamba marehemu alipokua anatoka bafuni kwa kujiandaa kutoka Ijumaa usiku wa kuamkia Jumamaosi kwenye saa 6 usiku alimsikia Lulu akiongea na mwananume mwingine kwenye simu ndipo ilipotokea purukushani [...]
MSANII mahiri wa filamu za kibongo, Hemed Suleiman ‘P.H.D’, amesema kuwa majivuno ni sababu moja wapo inayochangia kwa kiasi kikubwa kushusha ubora wa filamu Tanzania.
Alisema kuwa wasanii wengi baada ya kucheza filamu kadhaa wanaanza kujiona tayari wametoka na hata wakiitwa kucheza filamu fulani ambayo haina nyota wengi wakubwa wanakataa.
Aliongeza kuwa kwa upande wake hawezi kukataa [...]
MSANII wa bongo movie Ndumbangwe Misayo ‘Thea’, amesema kuwa mwezi huu wa April anatarajia kuachia filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Zawadi ya Christmas’, ambayo itakuwa na nyota kibao wa tasnia hiyo.
Aliwataja baadhi ya wasanii waliocheza katika kazi hiyo kuwa ni Stara Thomas, Adam Kwambiana, Single Mtambalike ‘Rich Rich’ na wengine kibao.
Akiongea na DarTalk, [...]
BAADA ya kufanya vizuri ndani ya bongo movie, wasanii Salma Jabu ‘Nisha’, na Frola Mvungi, wameamua kuingia katika fani ya muziki, wanajipanga kuja na ngoma yao ya kwanza itakayokwenda kwa jina ‘Sinaga’, wakiwa wamemshirikisha rapper Mo Racka.
Akiongea na DarTalk, Nisha alisema kuwa ngoma yao ni kali na lengo lao ni kuja kufunika. Wasanii hao wameunda [...]
MTUNZI wa vitabu na filamu bongo, Aunty Fifii, amesema kuwa kitabu chake cha ndoa kilichopewa jina la ‘Migogoro ya Ndoa na Suluhisho lake’, kinatarajia kuingia sokoni rasmi mwezi huu wa April mwaka huu kwa mujibu wa ratiba walizopanga ingawa tarehe kamili bado haijajulikana.
Akiongea na DarTalk, mtunzi huyo mwenye jina kubwa Tanzania na Afrika kwa ujumla, [...]
MSANII kutoka bongo movie Christine John ‘Sintah’, ameuambia mtandao wa DarTalk, kuwa amepata kipindi kwenye redio Times FM, hivyo mashabiki wake wataweza kumsikiliza katika redio hiyo.
Alisema kuwa hata hivyo anaamini ataendelea na kipaji chake hicho kwani ni kazi ambayo anaiweza kuliko nyingine zote ambazo amekuwa akifanya.
Hata hivyo mwandishi wa habari hizi alimuuliza swali msanii kuwa [...]
MSANII anayetamba na ngoma ya ‘Dume Dada’, Shilole amesema kuwa filamu yake ya ‘Shilole In Dar’, inatarajia kutoka mwezi Mei mwaka huu.
Alisema kuwa kwa mwezi huu wa April atakuwa katika mchakato kupiga picha kwa filamu hiyo, kwani anaamini haitachukua muda mrefu kukamilika.
Alidai kuwa ndani ya filamu hiyo hakutakuwa na wasanii hata mmoja mwenye jina kubwa [...]
MTAYARISHAJI wa tamthili na filamu Tanzania, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuzi’, ameuambia mtandao wa DarTalk, kuwa filamu yake ya ‘Tatakoa’, imetumia sh mil 18, na sasa ipo katika hatua za mwisho kutoka.
Mr Chuzi alisema kila kitu kimekamilika na kikubwa kinachoendelea sasa ni uhariri na baada ya hapo wataizindua ili mashabiki wao waweze kujua ni kitu gani kinachokwenda [...]
MSANII aliyetamba na ngoma ‘Mpenzi Bubu’, H-baba, amesema kuwa hakuna bifu lolote linaloendelea kati yake na Mr Chuzi, kwani ni watu ambao wapo karibu siku zote.
Mtandao wa DarTalk, ulimuendea hewani msanii huyo baada ya tetesi kutoka kwa mpenzi Frola Mvungi kuwa ametongozwa na Chuzi kitu ambacho kwa upande wake H-Baba ameweka wazi na kusema hakuna [...]