
WAKATI ngoma yake ya ‘Chukua Time’ ikiendelea kushika chati za juu, msanii Suma Mnazaleti, amesema kuwa watu wengi wamekuwa na hamu ya kutaka kumjua ni msanii wa bongo movie anayemzungumzia katika ngoma hiyo, lakini anashindwa kumtaja kwani tangu alipokuwa anaandika wimbo huo alikula kiapo kuwa hatokuja kumtaja jina kamwe.
Mnazaleti alizungumza na DarTalk kuhusu jina la staa wa bongo movie [...]
MSANII wa muziki wa kizazi kipya bongo Samir, ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ‘Sina Raha’ , ameweka wazi kuwa kuna wakati alikuwa kimya kwenye game na hapo ndipo alipowangudua rafiki wa kweli na rafiki ambao humpenda hadi pale anaposhika chati, kitu ambacho kimefanya kuwa makini katika hilo.
Kauli ya msanii huyo imekuja mara baada ya kuzungumza [...]
MSANII wa muziki wa kizazi kipya bongo anayefanya Hip Hop, Dan Rock, amesema kuwa sasa anakuja na ngoma mpya ya ‘Kitola’, akiwa amemshirikisha bingwa wa miduara, AT.
Msanii huyo tayari ngoma yake ya ‘Muda Umewadia’, alichomshirikisha Maunda Zorro, imeweza kumweka katika kiwango fulani katika muziki ingawa bado ana changamoto nyingi za kuweza kupigana na kufika juu zaidi ya alipo [...]
Behind the Scenes of Video Shoots for Wakazi upcoming songs in ABACUS EP. Be on the lookout for for debut of “Taking Over the Game” followed by these videos that are in the works.
Rais wa TAFF Simon Mwakifwamba
SHIRIKISHO la filamu Tanzania TAFF, limetoa tamko kwa wasanii wake hasa wale wanaoendelea kufanya vitendo vya uvunjaji wa maandili kuwa wanasuburi sheria kutoka BASATA, ili waaze kuchukua hatua za kinidhamu.
Akizungumza na mtandao wa DarTalk Rais wa TAFF, Simon Mwakifwamba, alidai kuwa wanasikitishwa na tabia ambazo zinanaendelea kufanywa na wasanii wake kwani vitendo hivyo vinawafanya hata wadau wa [...]
WAKATI baadhi ya mastaa bongo wakikataa kuolewa kwa sababu zao binafsi, mrembo anayetamba kwenye video za bongo Agnes Gerald maarufu kama Agnes Masogange, amedai kuwa kuishi bila mume kunamfanya aishi maisha ya raha, kwani anaamini akiolewa atakuwa kama mfungwa anayesubiri hukumu ya kifo.
Mwanadada huyo ambaye amekuwa akikumbwa na skendo kibao katika maisha yake, amedai kuwa maisha yake yanaenda [...]
MSANII anayefanya muziki kimataifa huku akiwa tayari ameshafanya na wasanii kibao wa nje, nchi kama USA, Nigeria, Kenya, Uganda na nyingine nyingi, Ambwene Yessaya ‘AY’, amesema kuwa anaamini kati ya wasanii wa bongo ambao wanaweza kufikia kiwango kikubwa kimataifa ni Ommy Dimpoz, kwani kila anapokuwa naye mara nyingi huwa anapenda kujua muziki wa nje unavyokuwa.
AY aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye televisheni [...]
MSANII wa muziki wa kizazi kipya bongo Becka Title, ameuambia mtandao wa DarTalk, kuwa anatarajia kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Nilisema’, ambayo kafanya na wasanii wawili Felly Kano na Pinda Bwai kutoka studio ya Masanjuo chini ya producer Kona.
Alisema kuwa baada ya kwenda hewani audio hiyo atakuwa katika maandalizi ya video yake hivyo anaamini kwa sasa mashabiki wake [...]
KAMA ni mtu wa kusikiliza ujumbe kwenye kazi za wasanii wa kibongo basi kwa R.O.M.A a.k.a ‘Mkatoliki’ huwezi kuukosa, ambapo amesema kuwa mara nyingi huwa hana haraka ya kutoa ngoma hovyo hovyo kwani kazi zake huwa zinatumia muda mrefu kuandika kwa sababu ya kutafuta ukweli wa mambo ambayo yanatokea kwa jamii yanazungumzwa n.k.
Roma amefanya vizuri na kuteka [...]
Madam Ritha akikata utepe katika uzinduzi rasmi wa EBSS House jana jioni.
Madam Ritha, Chief Judge akifungua mlango wa EBSS house rasmi baada ya sherehe ya uzinduzi kuanza.
Madam Ritha akiwatembeza viongozi wa Zantel ndani ya nyumba.
Madam Ritha akiwaonyesha wageni nyumba (Uongozi wa Zantel).
Washiriki walioingia Top 12 kwa pamoja wakiwakaribisha wageni baada ya mlango kufunguliwa.
Baadhi ya washiriki [...]