Category | What's New

09 January 2013

MSANII wa muziki wa kziazi kipya kutoka mkoani Morogoro Belle9, ameuambia mtandao wa DarTalk kuwa yupo mbioni kuachia ngoma mpya kwa lengo la kufungua mwaka ingawa ameshindwa kuweka hadharani jina la ngoma hiyo kwani anahitaji iwe kama zawadi kwa mashabiki wake.

Mwandishi wa DT alifanya mazungumzo na msanii huyo kwa lengo la kutaka kujua amejipanga vipi ndani ya mwaka huu, [...]

09 January 2013

MSANII anayekuja juu kwenye muziki wa bongo fleva Ally Nipishe, ameuambia mtandao wa DarTalk kuwa ameshakamilisha video ya ngoma yake ya ‘My’, na muda wowote itakuwa sokoni kwa lengo la kuwaonesha watanzania kile maana halisi ya jina la kazi yake.

Ally alisema kuwa baada ya audio yake kufanya poa aliona ni vibaya kuwa kimya kwenye upande wa video ndipo [...]

08 January 2013

Msanii aliyekuwa anafanya muziki aina ya Mnanda  na Mchiriku, Omary Omary amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Omary Omary aliyetamba na wimbo wake maarufu wa ‘Kupata ni Majaliwa’ alifariki nyumbani kwao Temeke saa chache baada ya kurejeshwa toka hospitali ya temeke alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa, Inasemekana kuwa mara baada ya [...]

06 January 2013

BAADA ya kudaiwa kuwa msanii Najana mahusiano ya kimapenzi na Diamond, sasa mwenywe ameamua kuweka wazi kuwa anamfahamu Diamond kama msanii na mara nyingi wanakutana studio tu na hana muda wa kuzungumza naye ishu nyingine kama watu wanavyozusha.

Naj alifanya mazungumzo ya dakika kadhaa na mwandishi wa DarTalk maeneo ya Coco Beach, ndipo alipoweka usawa juu ya ishu hiyo, [...]

06 January 2013

WAKATI vijana wengi wakikacha tukio la kufunga ndoa, msanii anayetamba na kibao chake cha ‘Bado Kijana’, Timbulo, amesema kuwa baada ya kuishi na mpenzi wake kwa muda mrefu sasa ameona ni vema kumchukua kabisa ili awe mke na mikakati hiyo imeanza kufanyika na muda wowote watu watakula pilau.

Timbulo alitoa ishu hiyo baada ya kuzungumza na mtandao huu, [...]

06 January 2013

WASANII wawili ndani ya muziki wa kizazi kipya The Super na Soc wanaounda kundi la Dar Money, wamesema kuwa wanatarajia kuachia audio na video ya ngoma yao mpya inayokwenda kwa jina la ‘Moyo hauna Macho’, waliyofanya na msanii kutoka Tip Top Connection, Tundaman.

Wasanii hao walifanya mazungumzo na mtandao huu ambapo walisema kuwa ngoma hiyo iko poa na hata upande [...]

04 January 2013

WAKATI wasanii wengi wakificha kusema ukweli walikoto hasa kwenye safari ya muziki, msanii anayefanya poa kutoka  Mtanashati Entertainment, Dogo Janja, amesema kuwa wakati alipokuwa akifanya muziki huko kwao Arusha baadhi ya Ma DJs walikuwa wakimpiga sana vibao kutokana na nyimbo mbovu alizokuwa anafanya.

Alisema kuwa aliwahi kufanya nyimbo zaidi ya saba alipokuwa Arusha lakini hazikuweza kufanya chochote ingawa alianza kupata [...]

04 January 2013

MSANII anayesikika na ngoma zake mbili ‘Sinyorita’ na ‘Mapenzi Mabaya’, Jay Mpole, amesema kuwa kikubwa kinachomuumiza kichwa katika muziki wake ni suala la kupata menejimenti itakayoweza kuendesha kazi zake zote za kimuziki.

Msanii huyo alizungumza na mwandishi wa DarTalk kwa lengo la kutoa ishu hiyo ili hata mashabiki wajue, ambapo alisema kuwa anafanya poa katika muziki lakini [...]

04 January 2013

WAKATI baadhi ya wasanii baada ya kupata hela kidogo wanakimbilia kununua magari huku bado wanakaa kwenye nyumba za kupanga, mkali kutoka Mbeya, Izzo Business, amesema kuwa anayajua sana magari ndiyo maana hatua ya kwanza katika maisha yake ameamua kujenga nyumba kwao Mbeya ambayo anaamini itamsaidi sana kuliko hata gari.

Mkali huyo alifanya mahojiano na mmwandishi wa DarTalk, ambapo ulitaka kujua [...]

02 January 2013

MSANII Tundaman baada ya kumcheka mwenzake Matonya na kumuimba kwenye wimbo wake kuwa alifungiwa ndani na mwanamke na kulizwa shilingi milioni 6, hali kwake imekuwa mbaya zaidi ambapo inadaiwa kuwa hivi karibuni amekombwa milioni 7 na mwanamke mmoja aliyelala naye na kujikuta akiwa hana hata chenji mfukoni.

Chanzo kimoja cha habari kilichozungumza na mwandishi wa DarTalk kwa sharti la [...]

SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!