08 May 2013

MWIGIZAJI Mahiri wa filamu Wema Abraham Sepetu ndiye msanii anayelipwa fedha nyingi kuliko msanii yoyote wa filamu katika kushiriki katika filamu kutoka kwa watayarishaji wengine ili uweze kumshirikisha Wema Sepetu katika filamu yako kama mwigizaji bila kujali anacheza scene ngapi gharama yake ni milioni kumi.

Wema ambaye kwa sasa anamiliki kampuni yake ya utengenezaji wa filamu inayojuklikana kwa jina la Endless Fame Films anasema kuwa moja ya sababu inayomfanya aweze kuchaji gharama hiyo inajumuisha na kutumia kampuni yake pamoja yeye mwenyewe kuigiza katika filamu hiyo, kwa hiyo ni wajibu wa mhusika kumudu gharama hizo.

“Yaah kama mtayarishaji ananihitaji kushiriki katika filamu yake atatakiwa kunilipa kiasi cha shilingi milioni kumi kwa kushiriki katika filamu yake, lakini pia kuzingatia ratiba ya utendaji usiingiliane na kazi zangu nyingine,”anasema nyota Wema.



Wema Sepetu akiwa na Chiddy Classic studio ofisini kwake.

Inasemekana kuwa Wema ndio msanii wa kike anayeuza filamu kuliko mwigizaji wa filamu wa kike, pengine ndio sababu ya kuweza kutoza gharama kubwa katika kushiriki filamu nje ya kampuni yake unapomuhitaji Wema kwa ajili ya mapatano unaongea na mtendaji wake wa karibu Chiddy Classic.

Gharama hizo ndio kubwa kwani hadi sasa msanii ambaye amelipwa kwa kiwango cha juu ilikuwa ni milioni tano ikiwa kama ndio kikomo cha malipo kwa wasanii wenye majina na wamiliki wa makapuni yao, msanii kama Ray the Greatest hanunuliki kwani si rahisi kushiriki nje ya kampuni yake ya RJ Company. [source: filamucentral]

08 May 2013

NIKKI MBISHI – NEEMA [NEY WA MITEGO]

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

08 May 2013

SUMA LEE – WANASEMA

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

07 May 2013

Timewreckordz na NK Production kutoka nchini Tanzania ndo maproducer wa mwimbo wa Mshiriki waTanzania kwenye shindano la BigbrotherAfrica,sho inayoonyeshwa nchi 54 barani Africa, Mshiriki huyo Julio sasa amerudi kwenye fani aliyobobea ya Mziki na ameshafanya kazi na wasanii kibao wa bongo kama Chege, Matonya, Cassim Mganga, Country Boy, Chidi Benz, Ukeme, Bskillz, Lamar, Lucci, Jokate, Robz..na wasanii wa nje na pia washiriki wa Bigbrother mwaka jana…Seydou Soumare (Angola) Eazzy First Lady (Ghana) kwenye studio tofauti nchini na album inatoka july baada ya mafanikio ya mwimbo huu wa bigbrother.

Madhumuni ya kutoa single hii ni kuwakilisha Tanzania na muziki wetu Africa na Dunia, Na pia nchi zenye kupendelea kuangalia Bigbrother ambao wafuatiliaji wa kipindi hicho cha miezi mitatu wako zaidi ya million 20,Huu ndo muda nchi yetu itasikika kirahisi kimziki kwa nchi 54 Africa kwasababu ya nyimbo kuwa kali na vigezo vyote na kwamba inahusiana na hiyo show….Nyimbo inaitwa ‘Mr Big Brother’ na inaoongelea big brother kama show, nchizi zinazoshiriki, Msiba tuliopata mwaka jana heshima kutoka kwa watanzania baada ya kumpoteza mshiriki mkubwa mwaka jana Goldie.

Huu ndio mwimbo wetu kwa mara ya kwanza katika historia ya bigbrother msanii kutoka nchini kutoa mwimbo kwa ajili ya Big Brother Africa na support ya watanzania itatufanya kufikisha mziki wetu nje ya Tanzania na Africa. Big brother mwaka huu inaanza baada ya wiki mbili 26/may/2013 .Tujivunie cha kwetu na kupeperusha bendera yetu Africa.

JULIO – MR. BIG BROTHER

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

07 May 2013

Baada ya story ya mwanadada Jacqueline wolper kutolewa nje pamoja na vitu vyake kuzagaa kwenye vyombo vya habari hususani magazeti, tuliamua kumtafuta mwanadada huyu ili tupate ukweli wa jambo hilo na kuamua kumtafuta hewani

Mwandishi: Mambo Jack, mzima wewe?

Jackline Wolper: Mi mzima, vipi salama?

Mwandishi: Salama kabisa, vipi kuhusu hii habari ya kutolewa vitu nje ya nyumba? Nini tena kimetokea?

Jacqueline Wolper: Hiyo habari sio ya ukweli kama ilivyo, ukweli ni kwamba sijatolewa vitu ila nimehama sehemu niliyokuwa nakaa na kuhamia sehemu nyingine



Nyumbani kwa Wolper anapoishi hivi sasa baada ya kuhama Mbezi Beach

Mwandishi: Kitu gani kilitokea mpaka kukawa na hizi habari za kutolewa vitu nje? Na ulikuwa unakaa wapi?

Jackline Wolper: Mwanzo nilikuwa nakaa ,Mbezi beach, kwenye apartment ya kama USD 1500 kwa mwezi, na nilikuwa nakaa mwenyewe, na kama unavyojua huwa nawalea wadogo zangu na muda huo walikuwa wapo chuo. Ila walipomaliza nikaona badala ya mimi kukaa mwenyewe ni bora nitafute nyumba nyingine mbili ili wakae wenyewe na mimi nikae mwenyewe.

Ndo maana nikahama huko mbezi beach. Sa sijui hao wanaosema nimetolewa vitu nje wanatoa wapi hayo maneno. Labda kama walipiga picha wakati nahama na kuamua kujitengenezea stori.

Mwandishi: Unahisi ni kwanini wameandika kuwa umetolewa vitu nje?

Jackline Wolper: Mmmh! Siwezi kujua na wala hainisadii, maana sio kweli. Mi sukuona sababu ya kulipa hizo hela kwa mwezi wakati naweza kukaa kwenye nyumba nzuri ya $800 au mia $900 kwa mwezi na nikawatafutia wadogo wangu nyumba nao wakae kwa gharama hiyo hiyo na kwa uhuru wao.

Kwangu mimi haina maana hata kidogo kwa sasa kulipa hela zote bila sababu, Wakati nipo mwenyewe ilikuwa sawa ila sasa it doesn’t make sense at all. Kuna mambo mengine ya muhimu ya kufanya. Na isitoshe suala la foleni. So sijui waliondika hivyo wanatafuta nini kwangu.

Mwandishi: Basi tunashukuru sana Jack kwa maelezo yako.

Jackline Wolper: Asanteni sana

source: bongomovies.com

06 May 2013

Pata new joint toka kwa Mc Gozzo akiwa na Legendary JCB ndani ya ngoma hii ikiwa beat ni mkono wa Kazawaza Records na vocal la Noizmekah Productions Arusha chini ya producer dx aka defxtro,Ngoma inakwenda kwa jina ‘Shika’. Download HAPA and keep Supporting African Music..Powered by www.vmgafrica.com

GOZZO FT JCB – SHIKA

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

06 May 2013

JOSLIN – ITIKA

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Page 12345678910203040...

SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!