
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Timbulo, ameonekana kuvuta hisia za watu wengi kwenye mitandao ya kijamii na kuacha maswali mengi baada ya kuonekana akiwa na msanii wa filamu Rose Ndauka kwenye pozi tata chumbani huku Ndauka akiwa amevaa taulo na hapo ndipo utata huo unapokuja.
Timbulo kutokana na picha hiyo inachora ramani tata, ambayo itamweka kwenye wakati mgumu kutokana na mashabiki wake wengi kuhisi walikuwa kwenye hisia kali za mapenzi hasa uvaaji wa taulo wa Ndauka tena wakiwa kitandani.
DarTalk baada ya kupata picha hiyo ilimtafuta Timbulo na kuzungumza naye ambapo, alidai kuwa picha hiyo imepigwa wakati wakishuti filamu ambayo wao wote wameshirikishwa na hapo hakuna ubaya wowote ulifanyika.
“Dah nashindwa kueleza kwani picha ni kweli tulikuwa chumbani na hakuna kitu kilichotokea zaidi amani tu, na nachoweza kusema watu walihisi mimi natoka na Ndauka ila siyo hivyo ingawa nampenda sana huyo dada,” alisema.
MKALI wa muziki wa Hip Hop anayetokea mkoani Morogoro Afande Sele, ambaye kwa muda mrefu hajaonekana kwenye video sasa amesema kuwa yupo kwenye harakati za kuipeleka ngoma yake ya ‘Soma Ule’ kwenye kideo ikiwa ni awamu yake ya kwanza ndani ya mwaka ya kutengeneza video.
Afande alizungumza na mwandshi wa DarTalk ambapo alisema kuwa mwaka huu ameona ni vyema kuwapa kile wanachokitaka mashabiki wake, ambapo wengine wamekuwa wakitaka kumuona kwenye video badala ya kumsikia kwenye audio pekee.
Alisema video hiyo inatarajia kufanywa na kampuni ya ShowBiz Defined, ambapo tayari mazungumzo yamefanyika na sasa anasubiri siku ambayo wataanza kupiga picha za ngoma hiyo.
“Natarajia kuanza kuonekana kwenye video yangu ndani mwaka huu na sasa tayari mchakato wa kupiga picha ngoma yangu unafanywa hivyo mashabiki wa kazi zangu nimeskia kilio chenu muda wowote kazi itakuwa tayari,” alisema.
Hata hivyo alipoulizwa juu ya kutoa albamu, alisema kuwa nalo amekuwa akilifikilia kwa muda mrefu, hivyo ndani ya mwaka huu anaweza kuachia albamu, na hatojali suala la mauzo au soko kwani anachohitaji ni kuwapa elimu mashabiki wake.
“Sitofikiria soko kama litalipa ama vipi nachohitaji ni kuwapa elimu watanzania, na wengi wamekuwa wakinitumia ujumbe kwamba wanataka albamu hivyo nachoweza kuwaambia ni kwamba mwaka huu watapata albamu yangu tena ikiwa na ngoma kali,” alisema.
SHO DADDY – MAKELELE
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
MSANII wa filamu na ambaye pia aliwahi kuwa mtangazaji wa TV Aunty Lulu, amesema kuwa anajuta ni kwa nini alishawishika kuigia kwenye tasnia hiyo ya filamu kwani ni bora angeendelea na kazi yake ya awali, kwani huko kumemfanya aonekane kama changundoa wakati hayuko hivyo.
Tasnia ya filamu imekuwa ikiwaharibu vijana wengi hasa wakike wanaopenda kufanya kazi hiyo na mwisho wa siku wanaonekana kama wamepoteza muelekeo wa maisha, kutokana na anasa zilizopo ndani ya tasnia hiyo.
Aunty alisema kuwa awali kabisa alipenda kufanya kazi hiyo lakini kadri siku zinavyokwenda mbele anajiona wazi kuwa amebandilika na amekauwa na tabia chafu ambazo hazina mfano.
Alidai kuwa inawezekana hakujua namna ya kujipanga pindi alipokuwa anaigia kwenye tasnia hiyo, lakini sasa anaona wazi kuwa tayari ameshazama kwenye shimo na kutokana kwake ni vigumu kwani hayo ya sasa ndiyo maisha aliyozoea.
“Awali sikuwa hivi asa sijui hii ni kwa sababu ya kuingia kwenye filamu au vipi, lakini kuna matukio mengine nimeyafanya ambayo kwa kweli si mfano wa kuigwa,” alisema.
YOUNG DEE FT MR. BLUE – HUJALI
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
WAKATI akizidi kukimbiza kwenye game la muziki, msanii Shilole, amefunguka kuwa wanaomchukia wanendelee kumchukia na yeye atazidi kufanya kazi ambapo sasa yupo mbioni kuipua mzigo mpya unaokwenda kwa jina la ‘Marry Maria’, akiwa sambamba na baba ya muziki Dully Sykes.
Shilole amekuwa akiandamwa na wasanii kadhaa lakini kutokana na kujua anachofanya kwa ajili ya mashabiki wake amekuwa akishindwa kuwajibu kwani haitaji kupoteza muda wake, badala yake nguvu zake anazipeleka zaidi kwenye kazi.
Mwandishi wa DarTalk, alimtafuta msanii huyo ili kupiga naye story kadhaa, ambapo alizungumzia ujio wa kazi hiyo na kudai kuwa ngoma ipo mbioni kwenda sokoni na anaamini itakuwa kwenye kiwango kikubwa kwani msanii aliyefanya naye ana kiwango kikubwa.
Alisema kuwa ujio wa kazi hiyo ni moja ya kuanza ratiba zake za kufanya show za kimataifa, ambazo zitaweza kumkuza zaidi kimuziki, ingawa hakuweka wazi ni nchini gani ataenda kupiga show hizo.
“Mzigo unakuja na kazi imetengenezwa kwenye kiwango kikubwa, sambamba na ujio huo pia natarajia kufanya show za kimataifa na kwa wale wenye chuki wataumia sana mwaka huu sina muda wa kujibu watu zaidi ya kufanya kazi,” aliongeza.
MSANII wa filamu na muziki Snura Mushi ‘Snura’, anayetamba kwa mauno, ameeleza kuwa mwaka huu anaamini ni mwaka wake wa kukimbiza kutokana na mapokezi makubwa anayoendelea kuyapata kutoka kwa mashabiki wake hasa kwenye show zake.
Snura alizungumza na mwandishi wa DarTalk, ambapo alisema kuwa muziki wake umeedelea kumweka juu, na anaamini ujio wake wa mwaka huu kila msanii anayemfuata nyuma yake atasubiri kwani anajua kile anachokifanya kwa akili ya mashabiki wake.
Hata hivyo alisema kuwa anatarajia kuzindua rasmi video yake mpya ya ‘Majanga’ kwenye usiku wa Viuno Show ndani ya New Maisha Club Jumapili hii ambapo pia atasindikizwa na wakali wengine kibao.
“Nafanya muziki na filamu na huwezi amini mashabiki wangu wamekuwa wakipokea kwa shangwe sana pale napoenda kufanya show, naamini huu mwaka kwangu utakuwa na mafanikio makubwa sana tofauti na nyuma,” alisema.