04 January 2013

MSANII anayesikika na ngoma zake mbili ‘Sinyorita’ na ‘Mapenzi Mabaya’, Jay Mpole, amesema kuwa kikubwa kinachomuumiza kichwa katika muziki wake ni suala la kupata menejimenti itakayoweza kuendesha kazi zake zote za kimuziki.

Msanii huyo alizungumza na mwandishi wa DarTalk kwa lengo la kutoa ishu hiyo ili hata mashabiki wajue, ambapo alisema kuwa anafanya poa katika muziki lakini kikubwa ni timu ya kumsimamia hajapata kwani hawezi kufanya kazi zote pekee yake.

“Muziki ni usimamizi usione nyota wakubwa wa mbele wanafanya pouwa ukahisi wanafanya wenyewe wana utawala imara unaosimamia kazi zao, lakini hata hivyo nafanya mazungumzo na watu kadhaa ili tujue itakuwaje,” alisema.

04 January 2013

WAKATI baadhi ya wasanii baada ya kupata hela kidogo wanakimbilia kununua magari huku bado wanakaa kwenye nyumba za kupanga, mkali kutoka Mbeya, Izzo Business, amesema kuwa anayajua sana magari ndiyo maana hatua ya kwanza katika maisha yake ameamua kujenga nyumba kwao Mbeya ambayo anaamini itamsaidi sana kuliko hata gari.

Mkali huyo alifanya mahojiano na mmwandishi wa DarTalk, ambapo ulitaka kujua ni hatua gani aliyopiga katika maisha yake, ndipo alipofunguka kuwa hakuwa na tamaa kama za wasanii wengine za kununua magari na alichofanya kwanza ni kundondosha mjengo ambao anaamini utamsaidia maisha yake yote.

Alisema kuwa alitaka kununua gari lakini aliona ni bora kwanza aweke nyumba yake sawa ili hata baadaye atakapohitaji kujenga familia yake asianze kupanga kama wengine wanavyofanya.

“Magari yapo lakini kupata nyumba ni vigumu sana napenda gari ila kwa sasa najiamini kwamba mjengo wangu upo hata napoenda nyumbani nafikia kiwangu si kwa wazazi tena, nyumba hiyo naamini itanisaidia miaka yote tofauti na gari ambalo linakuwa na matatizo mengi,” alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa wapo baadhi ya wasanii ambao hupata fedha nyingi lakini hawaamini kama kuna kujenga na tamaa zao kubwa ni kununua magari ya kifahari kila siku huku mwisho wa siku wanalala kwa marafiki.

04 January 2013

DOCHI FT ALIKIBA – IMANI

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

02 January 2013

MSANII Tundaman baada ya kumcheka mwenzake Matonya na kumuimba kwenye wimbo wake kuwa alifungiwa ndani na mwanamke na kulizwa shilingi milioni 6, hali kwake imekuwa mbaya zaidi ambapo inadaiwa kuwa hivi karibuni amekombwa milioni 7 na mwanamke mmoja aliyelala naye na kujikuta akiwa hana hata chenji mfukoni.

Chanzo kimoja cha habari kilichozungumza na mwandishi wa DarTalk kwa sharti la jina lake kutotajwa kilidai kuwa, msanii huyo alikuwa na sh milioni 7 ambazo alizipata kwenye moja ya show alizofanya hivi karibuni.

Mhabishaji huyo alisema kuwa baada ya kupata kiasi hicho cha pesa alisita kwenda kulala kwa rafiki yake Madee ndipo alipoamua kwenda kwa mwanamke huyo kwa lengo kutunza fedha hizo bila kuchukua tahadhari yoyote na fedha hizo, kitu ambacho kimempelekea kupoteza fedha zote huku mwenyewe akiwa kimya kwa hofu ya kuchekwa.

“Jamaa hadi leo kimya hafanyi tena mchezo wa kwenda kulala na demu na mshiko mrefu kwani kilichomkuta anajuta ni kwa nini alimuimba Matonya kwenye wimbo wake,” kilidai chanzo hicho.

02 January 2013

WAKATI wasanii wengi wakichemsha kwenye show, mkali kutoka THT, Amini, amesema kuwa anamkubali Diamond kwenye upande wa show kwani anavuta mashabiki wengi kuliko msanii mwengine yeyote Tanzania.

Kauli ya msanii huyo aliitoa jana kwenye usiku wa Wasafi ambapo Diamond alikuwa akipiga show New Maisha Club, ambapo watu wengi waliojitokeza kwa lengo la kuona msanii huyo anafanya nini ndani ya usiku wake.

Amini alisema kuwa kutokana na umati uliojitokeza haamini kama kuna msanii mwingine anayeweza kujaza club hiyo kama alivyofanya Diamond kwani watu walikosa sehemu ya kukaa huku wengine wakiishia kubaki nje.

“Hapana watu ni wengi sana na naamini Diamond kwa sasa kwenye upande wa show yuko safi sikutarajia kama watu wanaweza kujaa kiasi hiki, na si hapa show zake nyingi jamaa anafanya poa namkubali sana,” alisema.

02 January 2013

MSANII wa filamu aliyekuwa akisumbuliwa na homa kwa muda mrefu Juma Kilowoko ’Sajuki’, aliyefariki leo kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili anatarajia kuzikwa Ijumaa hii kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Saam saa saba mchama kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na ndugu wa marehemu.

Hata hivyo wasanii mbalimbali wa tasnia ya filamu na muziki pamoja na ndugu jamaa na marafiki na viongozi wa Serikali, wamezidi kujitokeza kwa wingi katika msiba huo uliopo Tabata kwa lengo la kuungana na watanzania wengine kuomboleza kifo cha msanii huyo.

Hata hivyo baadhi ya viongozi waliodhuria kwenye msiba huo ni pamoja na Mh January Makamba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli. Pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, alifika katika msiba huo ambapo alitoa salamu zake za rabirabi pamoja sh mil 1.

Pia Ruge Mutahaba ambaye ni mmoja wa Wakurugenzi wa Clouds Media Group huku akiwa ni mdau mkubwa wa tasnia ya burudani nchini Tanzania, alitoa salamu zake rabirabi na kiasi cha sh laki 5, huku akisisitiza kuwa tasnia hiyomimempoteza mmoja wa wasanii mahiri ambao nafasi zao haziwezi kuzibwa na mtu yeyote.

Hata hivyo baadhi ya wasanii waliowahi kufanya kazi na msanii huyo walisema kuwa kifo cha mwenzao ni pigo kubwa kwani hali yake ilianza kutengamaa lakini kutokana na mipango ya Mungu hawana budi kumuombea lakini wanaumia kwa kumpoteza mtu aliyekuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya filamu.

02 January 2013

MONSTER – SIJAWASUSA (VUMILIA)

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

02 January 2013

MSANII wa filamu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu. Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala, Rajabu Amiri ni kwamba hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen!

01 January 2013

MSANII anayekuja juu kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya kutoka visiwani Zanzibar, Saynag, amesema kuwa anawashukuru watanzania kwa kumpokea kwa mikono miwili kwenye game kwani anaamini ujio wake kutoka Visiwani hadi Bara umetokana na kazi ya muziki.

Msanii huyo ambaye amefanya ngoma kadhaa ikiwemo ‘Nafsi Inauma’, ‘Hisia Zangu’ aliyompa shavu Diamond, na nyingine, mtandao huo ulizungumza na msanii huyo ili kujua anakauli gani ya kuwapa mashabiki wake ambao wamempokea kwa shangwe na kumfanya awe juu, ambapo alisema kuwa hana kubwa sana ingawa anaamini wao ndiyo waloimfanya afike hapo alipo sasa.

Alisema kuwa watanzania wameweza kumpokea kwa shangwe ingawa hana cha kuwalipa zaidi ya kazi zake ambazo zinawa burudisha na kuwafanya wawe na furaha muda wote, lakini pia anaamini uwezo wake ndiyo uliochangia apokelewe vizuri.



Saynag stejini

Hata hivyo aliongeza kuwa pamoja na yote bado ana jukumu kubwa la kuongeza kasi katika kazi ili azidi kuwapa raha mashabiki wake wa Bara na Visiwani, ambao wanatumia muda wao kusikiliza kazi zake.

Naamini watanzania wanapenda sana muziki na wanampenda msanii anayefanya kazi nzuri, wamenipokea kwa mikono miwili, hivyo natoa pongezi zangu kwao kwani bila wao leo nisingekuwa hapa pengine bado ningekuwa chini sana,” alisema.

Hata hivyo mwanadada huyo mwenyewe uwezo wa kukata mauno, alisema kuwa mikakati yake ndani ya mwaka huu ni kufanya kazi nyingi na wasanii wakubwa ili azidi kujiweka kwenye chati sambamba na kutengeneza kazi zenye ubora wa hali ya juu.

01 January 2013

ELLIE GOULDING - LIGHTS (J-RYDER REMIX)

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!