04 June 2013

Mwili wa Marehemu Albert Mangwea aliyefariki dunia May 28 huko Johannesburg leo umeingia Dar es salaam na kupelekwa moja kwa moja hospitali ya Muhimbili, umati wa watu umefika uwanja wa ndege kushuhudia.

03 June 2013

KAMATI ya Mazishi ya aliyekuwa Msanii wa Bongo Fleva, Albert Mangwea ‘Ngwea’, mpaka jana mchana ilikuwa imekusanya jumla ya Sh milioni 32 kutoka kwa wadau mbalimbali.

Kamati hiyo inahitaji Sh milioni 50 kwa ajili ya kusaidia kusafirisha mwili wa marehemu kutoka Afrika Kusini mpaka Morogoro kwa ajili ya mazishi. Fedha hizo pia zinahitajika kwa ajili ya kuratibu shughuli nzima ya mazishi.

Mangwea alifariki dunia Jumanne iliyopita nchini Afrika Kusini akiwa usingizini kwa madai ya kuzidisha matumizi ya madawa ya kulevya.

Alitarajiwa kuwasili nchini jana lakini kushindwa kutoka kwa ripoti ya uchunguzi wa madaktari kwa wakati, kumesababisha isijulikane atatua lini, licha ya kudaiwa kuwa anaweza kutua leo.

Kamati ya Mazishi bado inaendelea na mchakato wa kuratibu shughuli hiyo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mwandishi akiwa Mbezi Goig jijini Dar ambako ndiko kwenye msiba huo, mmoja wa waweka hazina wa kamati hiyo, Paul Matthysse ‘P-Funk’, alisema mpaka sasa kamati yake imefikisha Sh 32,259,000 ingawa wanatarajia kuendelea kupokea michango mbalimbali kutoka kwa wadau.

Miongoni mwa watu wa kwanza kutoa michango yao katika msiba huo ni P-Funk aliyetoa Sh milioni tano, Clouds Media Group shilingi milioni tano na Push Mobile shilingi milioni tano.

Juzi Kampuni ya Global Publishers ilitoa shilingi milioni moja. “Nawasisitiza Watanzania waendelee kutoa michango yao kwa ndugu yao ili kuonyesha umoja tulionao. Fedha zikiwa nyingi tunataka kumfanyia kitu mama yake ili kuendelea kumfariji kwani kipindi hiki ni kigumu kwake,” alisema P-Funk.

Wakati huohuo jana taarifa zilisema mama mzazi wa Mangwea aishie Morogoro, Denisia Mangwea, alipandwa na presha baada ya jana kupata taarifa kuwa mwili wa mwanaye umezuiwa Afrika Kusini kutokana na uchunguzi wa madawa ya kulevya. Alikimbizwa hospitali na inadaiwa anaendelea vizuri.

Mangwea aliwahi kutamba na nyimbo kadhaa kali zikiwemo ‘Ghetto Langu’, She Got a Gwan’, Mikasi’ na Tupo Juu’.

03 June 2013

CHIKU K - SAUTI YANGU

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

03 June 2013

BECKA TITLE FT MIRROR & MR. BLUE – USIKU WA LEO

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

02 June 2013

TEAM DIGITAL VIBES [MOROGORO] – GOODBYE

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

ARTISTS:
BELLE 9, BIG POPPA, FREDRICK MULLA, YOUNG TUNDA, KOBA MC, CONSCIOUS, KACCI, STONE & PRINCE S.A.B!!

01 June 2013

COUNTRY BOY, P BLING, CHIBWA, TASH – R.I.P NGWAIR

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

31 May 2013

ALBERT MANGWEA [NGWEA] TRIBUTE MIX – HOSTED BY DJ NESTAR

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

31 May 2013

Jinsi ya kuchangia pesa kwa ajili ya kufanikisha mazishi ya Marehemu Albert Mangwea, kwa yeyote uliyeguswa na msiba wa msanii, ndugu yetu Albert Mangwea unaweza kuchangia pesa kufanikisha mazishi kwa kutuma chochote ulichonacho kupitia akaunti hii hapa …

ACC: NMB 2012505840 ambayo ni akaunti ya kaka yake anayeitwa KENNETH MANGWEA … Tigo Pesa 0717 553905. M PESA 0754 967738 zote ni namba za kaka wa marehemu.

Msiba uko wa marehemu uko Mbezi Beach Goig, Dar es salaam … Kituo cha kutokea MWENGE, utaona kibao kinachoelekeza au unaweza kuuliza na kuelekezwa. R.I.P Albert Mangwea!!

Page 12345678910203040...

SEARCH DARTALK

Copyright © 2011. DarTalk.com . All Rights Reserved. Site by NEXUS  |   BACK TO TOP!