Picha: Diamond Platnumz Akifanya Mazoezi Na Bendi Kujiandaa Na ‘tour’ Yake Na Ne-yo

Mwanamuziki Diamond Platnumz ameweka picha kwenye ukurasa wake wa Instagram zikionyesha akifanya mazoezi ya uimbaji akiwa na bendi yake ya muziki akieleza kuwa anajiandaa kwa ajili ya matamasha yake (music tour) yanayokuja hivi karibuni.

Katika picha hizo, Diamond aliandika “About [email protected]_wasafi HQ rehealsing for my upcoming Tour.”

diamond_platnumz

diamond_platnumz2

diamond_platnumz3

diamond_platnumz4

diamond_platnumz5

diamond_platnumz6

Diamond Platnumz anatarajia kufanya ‘tour’ ya muziki nchini Uingereza akiwa na mwanamuziki Ne-Yo siku za karibuni. Lakini pia alisema kuwa maandalizi ya kuimba na bendi sio tu kwa ajili ya ‘tour’ hiyo kwani hata kwenye matamasha mengine atakuwa akiimba ‘live’.

Aidha, alieleza kuwa alichelewa kuanza kutumia bendi kwa sababu alikuwa akitaka apate wapigaji vyombo wenye ujuzi. “Unajua wakati mwingine unaweza ukawa unaimba na bendi lakini ukaonekana unaimba vibaya sababu ya upigaji mbaya wa vyombo, mimi sikutaka hilo ndio sababu ilinichukua muda ili nipate watu wazuri,” alisema Diamond Platnumz.