Picha ya Aunty Ezekiel na Moses Iyobo Ikionyesha Ujauzito Yawa Gumzo Mtandaoni…!!

Moja kati ya picha ambazo zimekuwa zikisambaa kwa kasi katika mtandao wa Instagram leo Jumamosi ya November 26 ni picha ya muigizaji Aunty Ezekiel pamoja na mpenzi wake Mose Iyobo.

aunty_ezekiel

Picha hiyo ambayo imepostiwa na baadhi ya watu ikiwemo Mose Iyobo mwenyewe inamuonesha Aunty Ezikiel akiwa mjamzito, kitu ambacho kimefanya baadhi ya mashabiki wao kutoa comment za pongezi.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Mose Iyobo na Aunty Ezekiel wana mtoto wa kike anayejulikana kwa jina la Cookie hivyo kwa mujibu wa post ya Mose Iyobo inawezekana wakawa wanatarajia mtoto wa pili.